TRENDING DAILY POST | We Collect and Share Stories with you!

Kerosi ondieki ndiye spika wa kaunti ya kisii

0 comments



Kerosi ondieki ndiye spika wa kaunti ya kisii chini ya utawala wa ugatuzi baada ya kumbwaga chini ocharo kebira,okerosi alizoa kura za wawakilishi wa wadi 40 huku ocharo kebira akipata kura tano kwenye ujumuisho wa wawakilishi wa kaunti nzima ya kisii 45.

jaji mkuu wa mahakama ya kisii Ruth Sitati ndiye aliyeongoza shughuli ya kuwaapisha madiwani hao 45 ambapo baadaye walishiriki upigaji kura wa kumpata spika atakayeongoza shughuli na mipangilio ya kaunti.

Kerosi ondieki amekuwa wakili ndani ya mji wa kisii kwa muda sasa na pia mwenyekiti wa chama cha ODM kaunti ya kisii baada ya aliyekuwa mwenyekiti waziri chris mogere obure kuchaguliwa kuwa seneta wa kaunti ya kisii.

Baada ya kuchaguliwa kwake spika wa kaunti ya kisii okerosi ondieki aliahidi kuwatumikia watu na wenyeji wa kaunti ya kisii kwa uadilifu na vikamilifu kwa mujibu wa sheria zilizopo.

Ocharo kebira ambaye alibwagwa chini na okerosi kwa cheo hicho aliwania kiti cha eneo bunge la nyaribari masaba asifanikiwe kwenye kura zilizoisha hivi karibuni na akaamua kujaribu bahati yake kwa uspika wa kaunti aidha kwa tajriba yake ya uwakili.

Akizungumza kwenye hafla hiyo gavvana wa kaunti ya kisii James Ongwae amewataka madiwa waliochaguliwa na kuapishwa hii leo kujitolea kufanya kazi ili kuafikia malengo ya maendeleo yenye ufanisi walio ahidi nyakati za kampeini zao.

Waliokuwepo kwenye shughuli hiyo ni pamoja na wabunge Chris Bichage-nyaribari chache,Richard Onyonka-kitutu chache kusini ambaye pia ni naibu waziri wa wa maswala ya nchi za kigeni kando na naibu gavvana wa kaunti ya kisii Joash Maangi na viongozi wengine wa kiusalama ndani ya kaunti ya kisii.
Reported by Kobi Gilbert

 
Support : Disclaimer | Copyright © 2014. HOT STORIES ONLINE - Rights Reserved

Proudly powered by Blogger