TRENDING DAILY POST | We Collect and Share Stories with you!

KTN’S SENIOR INVESTIGATIVE REPORTER MOHAMED ALI OF JICHO PEVU PREDICTS HIS OWN DEATH IN THIS CHILLING LETTER DETAILING HIS POTENTIAL THREATS!!! HE MAY END UP LIKE JACOB JUMA

0 comments



“NIKIFA KESHO WENGINE WAJASIRI WATAZALIWA.
Huenda mada ya leo ikakutia hofu ama tumbo joto na kuwafurahisha wengine lakini usiwe na wasi wasi kwani kuzaliwa na kufa ni mapenzi yake Mwenyezi Mungu. Nikifa kesho msilie wala msinung’unike. Nikifutwa kazi kesho msiwe na chuki na mtu yeyote. Nikifungwa jela kesho msilie maana hii ndio safari ya mwanadamu ya kila siku. Msilie maana tulipofika sasa kama taifa tutalengwa wachache tunaopinga dhulma za kila siku. Tutalengwa wachache wanaopiga vita dhidi ya ufisadi. Tutalengwa kwa sababu tumekataa kuabudu miungu midogo midogo inayozidi kubaka taifa hili.

Tutazidi kulengwa kwa sababu tumekataa kula meza moja na wabakaji wa demokrasia. Leo hii waandishi wa habari wanakamatwa kiholela na polisi kwa sababu ya kufichua uhuni wa baadhi ya viongozi wanaojifanya watumishi wa wakenya ilhali tabia zao ni kama panya buku. Tabia ya kung’ata na kupuliza. Wanahabari wanaachishwa kazi katika njia isiyoeleweka kwa sababu ya kusimama imara na kupinga maovu ya serikali. Sisi tayari tumetia kichwa chetu maji kukabiliana na lolote lile litakalojiri kwa ajili ya kusimama na wakenya. Leo kila mmoja wetu aliye katika taaluma hii ni mlengwa.

Aliye katika afisi za serikali na anayepinga ukabila na wizi wa mali ya umma analengwa. Wengi wetu tunalengwa na kuzimwa ki-talanta kupitia wahuni wachache wanaojifanya wakubwa ila wao hawana tofauti na wale wanaobaka taifa hili, kwani ufadhili wa senti haramu za kuwapotosha wananchi kupitia taarifa bandia ndio kazi zao. Lakini leo nina habari njema kwa wakenya. Msiogope maana riziki yatoka kwake Mungu. Msiogope maana Mungu ni mkuu.
CONTINUE READING IN PAGE 2>>>
PAGE:  1,  2,  3,  4,  
 
Support : Disclaimer | Copyright © 2014. HOT STORIES ONLINE - Rights Reserved

Proudly powered by Blogger