TRENDING DAILY POST | We Collect and Share Stories with you!

KTN’S SENIOR INVESTIGATIVE REPORTER MOHAMED ALI OF JICHO PEVU PREDICTS HIS OWN DEATH IN THIS CHILLING LETTER DETAILING HIS POTENTIAL THREATS!!! HE MAY END UP LIKE JACOB JUMA

0 comments



Msiogope kudai haki zenu, mali yenu na uongozi mnaotaka. Msiogope kufutwa kazi kwa sababu ya kuunga mkono mabadiliko ya kweli. Hakika wengi wetu tutaumia katika safari hii ya kutetea nafasi yetu katika awamu ya tatu ya ukombozi wa Kenya. Awamu ya kuwaondoa wahuni wote mamlakani pamoja na wabakaji wa demokrasia. Mwaka wa 2017 utakuwa kama mwaka wa 2002 wakati ambapo vugu vugu litazaliwa kusafisha Kenya upya. Kesho ndio hiyo siku. Kesho yetu sote ni 2017. Kesho ni mimba ambayo imetungwa leo na yapaswa kujifungua.

Twatarajia kujifungua mtoto mzuri aliyetungwa na atakaeleta mabadiliko na wala sio starehe. Wakenya wana maono sasa na hakuna mtu yeyote atakayejaribu kusimama mbele ya vuguvugu la mabadiliko. Wakenya wanataka waheshimiwe na kulindwa na wala si kuibiwa kila kukicha.

Wakenya wanataka uongozi bora. Uongozi huo hautapatikana kwa kuwatesa baadhi ya watetezi wa haki za binadamu, wanahabari na wanasiasa wa upinzani. Hii itakuwa ni kosa kubwa kuwahi fanyika kwani wote hawa wanayafanya haya kwa minajili ya ukenya ndani yao na wala sio tamaa.

Safari ya mabadiliko imeanza na hakuna aliye na nguvu ya kuzuia wanayoyataka wakenya. Safari hii itakuwa ya kiu, mateso na machungu lakini hakika dakika ya mwisho sote tutashinda. Sote tutaungana na kusimama kama taifa. Wakuachishwa kazi wataachishwa, wakufungwa jela watafungwa, wakuuawa watauawa, wakuteswa watateswa lakini Kenya itasimama imara baada ya safari hii. Safari ya kutafuta demokrasia huwa chungu na iliyojaa mitihani.
CONTINUE READING IN PAGE 3>>>
PAGE:  1,  2,  3,  4,  
 
Support : Disclaimer | Copyright © 2014. HOT STORIES ONLINE - Rights Reserved

Proudly powered by Blogger