TRENDING DAILY POST | We Collect and Share Stories with you!

KTN’S SENIOR INVESTIGATIVE REPORTER MOHAMED ALI OF JICHO PEVU PREDICTS HIS OWN DEATH IN THIS CHILLING LETTER DETAILING HIS POTENTIAL THREATS!!! HE MAY END UP LIKE JACOB JUMA

0 comments



Hii ni safari waliopita watangulizi wenzetu kama vile marehemu Nelson Mandela, Mwalimu Julius Kabarage Nyerere, Jaramogi Oginga Odinga, Masinde Muliro, Martin Shikuku, Raila Odinga, JM Kariuki, Pio Gama Pinto, Tom Mboya, Field Marshal Dedan Kimathi miongoni mwa wakenya wengine wengi na mashujaa barani afrika.

Safari ya dhiki iliyoishia kuzaliwa kwa vyama vingi vya kisiasa mwaka wa 1991 kabla ya kuwaweka wakenya huru na kuwapa demokrasia ya kuuliza na kujibiwa kinyume na demokrasia dhalimu ya enzi za Jomo Kenyatta, Daniel Toroitich Arap Moi na sasa serikali ya madotcom kama wasemavyo iliyotutoa kutoka umaskini hadi ufukara.

Serikali inayotumia mabavu kwa kutueleza sisi wapiga kura eti ya kwamba watatutawala hadi mwaka wa 2032 pasi na kuona soni. Iwapo vitisho hivi vya hata kabla ya sisi kupiga kura si wizi basi ni nini? Unapowapata viongozi wenye damu moto na wakavu wenye kiu ya kupora mali ya umma, viongozi wa kujipiga kifua ya kutawala taifa basi jiandaeni maana mnaokaa nao meza moja ni sawia na fisi anayejifanya kuchunga kondoo kwa niaba ya mwenye boma. Mnaokula nao kwa jina la ukabila ni vipofu wabaya wanaoshika walaji wenza mikono wakikosa nyama.

Msiogope kufa, msiogope kuteswa maana kila dhulma haikosi mwisho. Leo nimeanza kwa kusema nikifa kesho kwa sababu najua unyama unaopangwa, najua hila chafu zinazopangwa dhidi ya wanaharakati wanaofanya kila wawezalo kukomboa Kenya upya. Hila hizi zimekuwa hatari kwa usalama maana zinatumiwa kwenye wino za ofisi mbali mbali nchini. Kwa wale wanaotaka wengine wafe kwa ajili ya kupinga miungu na makatuni wao nasema poleni maana yote yatakwenda kwa mapenzi na kudra yake mwenyezi Mungu. ‘
CONTINUE READING IN PAGE 4>>>
PAGE:  1,  2,  3,  4,  
 
Support : Disclaimer | Copyright © 2014. HOT STORIES ONLINE - Rights Reserved

Proudly powered by Blogger